Gurudumu la Uchumi
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.
- Indexed episodes, last 90 days
- 11
- Latest publication
- Sep 30, 2026
- Audience
- Checking…
- Earliest in this view
- Jul 8, 2026
Latest episodes
Kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu: mwanzo wa mapinduzi ya nishati Afrika Mashariki? (opens the original)
Read excerpt
Kenya inaagiza karibu mahitaji yake yote ya bidhaa za Petroli kutoka nje, hii ikiwa na maana kuwa bei na upatikanaji wa mafuta katika nchi hii, na kwa kiasi kikubwa katika ukanda unaweza kuathiriwa na mambo yanayotokea katika masoko ya kimataifa, hata hivyo habari njema ni kuwa bilionea wa Afrika Aliko Dangote anajenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu. Kwanini hatua hii ni muhimu? Tufuatilie
Hormuz na Bab el-Mandeb: Njia za baharini zinazotikisa uchumi wa dunia. (opens the original)
Read excerpt
Msikilizaji hebu fikiria mafuta unayoweka kwenye gari lako, bidhaa zinazofika kwenye maduka yetu kutoka Asia, mbolea inayotumika kwenye kilimo, au hata gharama ya kusafirisha kahawa na chai kutoka Afrika kwenda masoko ya nje, kwa namna moja au nyingine, sehemu ya uchumi huu inategemea bahari na kufungwa kwa njia ya Hormuz na sasa ile ya Bab el-Mandeb kunauweka uchumi wa dunia hatarini. Ungana nami kwenye makala ya wiki hii kufahamu zaidi.
Maisha mapya: Jinsi akina mama vijana wanavyobadilisha ujuzi kuwa fursa (opens the original)
Read excerpt
Nchini Kenya, suala la mimba za utotoni ni changamoto. Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya taofa nchini Kenya kupitia utafiti wa mwaka 2022 asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 walikuwa wamewahi kupata ujauzito. Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii, tunaangazia namna akina mama hawa wanavyogeuza ujuzi, juhudi na fursa za kiuchumi kuwa njia ya kujitegemea na kuwajengea watoto wao maisha yenye matumaini zaidi.
Umeme unaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki? (opens the original)
Read excerpt
Wikendi iliyopita, Tanzania ilizundua rasmi Mradi wa Umeme wa Maji wa bwawa la Julius Nyerere, lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115. Mradi huu, uliogharimu takribani shilingi trilioni 7.45 za Tanzania sawa na karibu dola za Marekani bilioni 2.9, unaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme. Katika Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunajiuluza Je, megawati hizi zitageuka kuwa uzalishaji, ajira, biashara na ukuaji wa uchumi?
Goma: Wanawake wapambana na umaskini licha ya changamoto za usalama. (opens the original)
Read excerpt
Msikilizaji katika mazingira ambayo migogoro na changamoto za kiuchumi zimeathiri maisha ya kila siku ya wananchi, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta njia mbadala za kujipatia kipato na kuendesha familia zao.Hali hii inashuhudiwa katika mji wa Goma, mashariki mwa DRC, ambako baadhi ya wanawake wamegeukia ufugaji wa kuku kama njia ya kujikimu, hasa baada ya shughuli za baadhi ya taasisi za kifedha kutatizika katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa AFC-M23.
Publishing over time
Last 90 days. Choose a month to open its work.
Recurring subjects
Named in the text we hold. One piece can cover several.
Not enough subject data for this period yet.
Audience
No verified audience measurement yet.
About this data
Counts cover the work we have indexed. Tone needs enough text and a confident classification. Excerpts and episode notes are not full articles or transcripts.
Identity or attribution wrong? Suggest a correction.